• HABARI MPYA

  Sunday, November 27, 2022

  AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 CHAMAZI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa 3-2 dhidi ya Coastal Union ya Tanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam.
  Katika mchezo huo mtamu wa ‘funga nikufunge’, mabao ya Azam FC yamefungwa na James Akaminko dakika ya 56, Yahya Zayd dakika ya 70 na Iddi Nado dakika ya 90 na ushei, wakati ya Coastal Union yamefungwa na Maabad Maulid dakika ya 14 na Hamad Majimengi dakika ya.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 32 katika mchezo wa 14 na kurejea nafasi ya pili, ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga SC ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Coastal Union baada ya kichapo cha leo wanabaki na pointi zao 12 za mechi 12 nafasi ya 12.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA COASTAL UNION 3-2 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top