• HABARI MPYA

  Sunday, November 27, 2022

  PHIRI APIGA MBILI SIMBA YAWAADHIBU POLISI MOSHI


  TIMU ya Simba SC imewaadhibu wenyeji, Polisi Tanzania kwa kuwachapa mabao 3-1 leo katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Ushirika mjini Moshi mkoani Kilimanjaro.
  Mabao ya Simba SC yamefungwa na washambuliaji, Nahodha John Bocco dakika ya 32 na Mzambia, Moses Phiri mawili, dakika ya 43 na 53, wakati la Polisi limefungwa Zuberi Mbogo dakika ya 90.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 31 katika mchezo wa 14 na kurejea nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao, Polisi Tanzania baada ya kipigo hicho wanabaki na pointi zao tisa za mechi 14 sasa nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI APIGA MBILI SIMBA YAWAADHIBU POLISI MOSHI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top