• HABARI MPYA

  Sunday, November 20, 2022

  IHEFU SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 UBARUKU


  WENYEJI, Ihefu SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali, Ubaruku mkoani Mbeya. 
  Mabao ya Ihefu SC leo yamefungwa na kiungo Mzimbabwe, Never Tigers dakika ya 41 na beki Mganda dakika ya 46, wakati la Coastal Union limefungwa na kiungo mshambuliaji, Mbaraka Hamza dakika ya 38.
  Kwa matokeo hayo, Ihefu SC inafikisha pointi nane katika mchezo wa 12, ingawa inaendelea kushika mkia, wakati Coastal Union inabaki na pointi zake 12 za mechi 11 nafasi ya 11.
  Mechi nyingine ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo, wenyeji Mbeya City wamelazimishwa sare ya bila mabao na Geita Gold Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Matokeo hayo yaanifanya kila timu ifikishe pointi 18, Mbeya City katika mchezo wa 12 nafasi ya sita na Geita Gold mchezo wa 13 nafasi ya saba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: IHEFU SC YAICHAPA COASTAL UNION 2-1 UBARUKU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top