• HABARI MPYA

  Thursday, November 17, 2022

  MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YAICHAPA SINGIDA 4-1


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wameibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Benjamin Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Yanga SC leo yamefungwa na mshambuliaji wake kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Fiston Kalala Mayele matatu, dakika za 16, 27 na 56 na beki wa pembeni, Kibwana Shomari dakika ya 48, wakati la SBS limefungwa na mkongwe, Meddie Kagere dakika ya 66.
  Kwa ushindi huo, Yanga SC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 10 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiizidi tu wastani wa mabao Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi, wakati Simba SC yenye pointi 24 za mechi 11 inashukia nafasi ya tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA HAT TRICK YANGA YAICHAPA SINGIDA 4-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top