• HABARI MPYA

    Saturday, November 26, 2022

    UCHAGUZI MKUU SIMBA SC KUFANYIKA MWAKANI


    MWENYEKITI wa kamati ya uchaguzi Simba, Boniface Lyamwike amesema uchaguzi Mkuu wa klabu hiyo utafanyika Januari 29, mwaka 2023.
    Katika taarifa yake ya leo, Lyamwike amesema; "Mwaka huu kanuni ambazo zitatumika kwenye uchaguzi wa Simba ni kanuni za Simba Sports Club. Huko nyumba tulikuwa tunatumia kanuni za TFF, katiba ya Simba ilikuwa inaruhusu."
    "Kanuni ya sita (kanuni za uchaguzi Simba), kigezo cha kwanza mgombea lazima awe mwadilifu na awe na kiwango cha juu cha uaminifu. La pili lazima awe mwanachama hai wa klabu."
    "Mtu yeyote ambaye anagombea nafasi ya mwenyekiti wa klabu ni lazima awe na angalau shahada ya chuo kikuu, na lazima awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha klabu ndani na nje ya nchi."
    "Anayegombea nafasi ya ujumbe wa Bodi ya Wakurugenzi lazima awe amefika kidato cha nne na cheti za kuhitimu, kigezo kingine awe mzoefu uliothibitishwa wa angalau miaka mitatu ya uongozi wa mpira wa miguu."
    "Kingine asiwe amepatikana kamwe ya hatia ya kosa ya jinai, lakini pia angalau awe na miaka 25 na si zaidi ya miaka 64, lakini pia asiwe mmiliki, mwanahisa au kiongozi wa timu ngyine ya mpira wa miguu."
    "Nafasi ambazo zitagombewa ni mwenyekiti nafasi moja, kutakuwa na mjumbe wa pili lakini pia kutakuwa na wajumbe wengine wanne. Jumla zitakuwa nafasi sita."
    "Katiba inampa nafasi mwenyekiti atakayechaguliwa kuchagua wajumbe wengine wawili. Lakini pia kuna kigezo cha msingi sana, katika nafasi nne, angalau mmoja au zaidi awe mwanamke." imemalizia taarifa ya Lyamwike.
    Kwa upande wake, Mjumbe wa kamati ya uchaguzi Simba, Dk. Gerald Mongela amesema
    Zoezi la kuchukua fomu litaanza Desemba 5, 2022 saa 3 asubuhi mpaka Desemba 19, 2022 saa 10 jioni. Fomu zitakuwa zinachukuliwa katika ofisi za klabu."
    "Desemba 20-21, 2022 itakuwa ukaguzi wa fomu zilizorudishwa ndani ya muda. Desemba 22-24, 2022 itakuwa ni usajili wa watia nia. Desemba 28, 2022 itakuwa kubandika majina ya wagombea waliopita kwenye usaili."
    "Desemba 29-20, 2022 tutatoa muda wa kupokea mapingamizi dhidi ya wagombea. Januari 1-2, 2023 itakuwa ni kupitia mapingamizi, kutoa wito kwa walioweka mapingamizi na wagombea waliowekewa mapingamizi."
    "Jan 3-4, 2023 tutakuwa na kipindi cha kusikiliza mapingamizi na kutoa uamuzi alafu Jan 5 tutatangaza majina ya wagombea. Jan 6-26 itakuwa dirisha la kampeni kwa waliopita kugombea na Jan 29 itakuwa uchaguzi." amesema Dk. Mongela
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: UCHAGUZI MKUU SIMBA SC KUFANYIKA MWAKANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top