// Disable text selection (not fully reliable)
function disableSelection(element) {
element.setAttribute('unselectable', 'on');
element.style.userSelect = 'none';
element.style.MozUserSelect = 'none';
element.style.webkitUserSelect = 'none';
}
// Apply to the entire document body
document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() {
disableSelection(document.body);
});
IHEFU YAZIMA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA MECHI YA 50 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINEIHEFU YAZIMA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA MECHI YA 50 - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
IHEFU YAZIMA REKODI YA YANGA KUTOFUNGWA MECHI YA 50
WENYEJI, Ihefu SC wamezima wimbi la Yanga kutopoteza mechi katika mchezo wa 50 baada ya ushindi wa 2-1 leo Uwanja wa Highland Estate huko Mbarali mkoani Mbeya. Haukuwa ushindi mwepesi, kwani ilibidi Ihefu watoke nyuma baada ya Yanga kutangulia na bao la Mchezaji Bora wa Ligi Kuu, kiungo Mkongo Yanick Bangala Litombo dakika ya tisa. Kiungo Mzimbabwe, Never Tigere aliifungia Ihefu SC bao la kusawazisha dakika ya 39, kabla ya Lenny Kissu kufunga la ushindi dakika ya 62. Kwa ushindi huo wa pili tu wa msimu kwa Ihefu iliyorejea Ligi Kuu baada ya msimu mmoja tangu ishuke, inafikisha pointi 11 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya 13 kwenye ligi ya timu 16. Yanga pamoja na kupoteza mchezo huo inaendelea kuongoza Ligi Kuu kwa pointi zake 32 za mechi 13 sasa, ikiizidi wastani wa mabao tu Azam FC ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
OMTO WAJA NA MAKUBWA 2024
-
Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts
Organization (OMTO), Anna Haule akizungumza wakati mkutano wa kwanza wa
mwak...
Reports: Jack Wilshere set for Arsenal return
-
Former Arsenal midfielder Jack Wilshere has held talks with the north
London side on one of its vacant academy coaching roles. Under 23 manager
Per Mertes...
YANGA ‘KUPAA’ JUMANNE KUIFUATA MWADUI FC
-
MARA baada ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Namungo Fc kwenye uwanja wa
Majaliwa, Lindi, siku ya jumapili, Kikosi cha Young Africans Sports Club,
kitareje...
0 comments:
Post a Comment