• HABARI MPYA

  Thursday, November 03, 2022

  SIMBA QUEENS YAFUFUA MATUMAINI YA KWENDA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA


  TIMU ya Simba Queens imeweka hai matumaini ya kwenda Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Wanawake Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Determine Girls ya Liberia jana Uwanja wa Prince Moulay Hassan Jijini Rabat nchini Morocco.
  Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Opa Clement dakika ya 53 na Olaiya Barakat dakika ya 80 kwa penalti, huo ukiwa ushindi wa kwanza wakitoka kufungwa 1-0 na wenyeji, FA Rabat kwenye mechi ya kwanza.
  Msimamo wa Kundi S sasa ni FAR Rabat inaongoza kwa pointi zake sita ikifuatiwa na Green Buffaloes na Simba Queens zenye pointi tatu kila moja, wakati Determine Girls inashika mkia ikiwa haina pointi.
  Mechi za mwisho za Kundi A Jumamosi patashika itakuwa kati ya Simba Queens na Green Buffaloes ya Zambia kila timu ikihitaji ushindi kwenda Nusu Fainali, wakati FAR Rabat inatarajiwa kuwa na shughuli laini mbele ya vibonde, Determine Girls.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YAFUFUA MATUMAINI YA KWENDA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top