• HABARI MPYA

  Thursday, November 10, 2022

  COASTAL UNION YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 PALE PALE SOKOINE


  WENYEJI, Tanzania Prisons wamepewa kichapo cha mabao 2-0 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Coastal Union yamefungwa na Maabad Maulid dakika ya tano na Hamadi Majimengi dakika ya 60 na kwa ushindi huo wanafikisha pointi 11 katika mchezo wa nane na kusogea nafasi 11.
  Kwa upande wao Tanzania Prisons baada ya kichapo hicho inabaki na pointi zake pointi 14 za mechi 11 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAICHAPA TANZANIA PRISONS 2-0 PALE PALE SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top