• HABARI MPYA

  Monday, November 28, 2022

  KAGERA SUGAR YAICHAPA MTIBWA 1-0 KIRUMBA


  BAO pekee la Meshack Abraham dakika ya 68 limeipa Kagera Sugar ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inayofundishwa na kocha na Nahodha wa zamani wa Mtibwa Sugar, Mecky Mexime inafikisha pointi 18 katika mchezo wa 14, ingawa inabaki nafasi ya tisa.
  Kwa upande wao, Mtibwa Sugar wanabaki na pointi zao 21 za mechi 14 sasa nafasi ya sita.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KAGERA SUGAR YAICHAPA MTIBWA 1-0 KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top