• HABARI MPYA

  Wednesday, November 16, 2022

  PHIRI AFUNGA BAO PEKEE SIMBA YAILAZA NAMUNGO 1-0


  BAO pekee la mshambuliaji Mzambia, Moses Phiri dakika ya 32 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Namungo FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 24 katika mchezo wa 11 na kusogea nafasi ya pili ikiizidi pointi moja Yanga ambayo hata hivyo ina mechi mbili mkononi, wakati Namungo FC inabaki na pointi zake 15 za mechi 11 nafasi ya nane.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: PHIRI AFUNGA BAO PEKEE SIMBA YAILAZA NAMUNGO 1-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top