• HABARI MPYA

  Saturday, November 19, 2022

  BOCCO APIGA HAT TRICK SIMBA YASHINDA 4-0


  MABINGWA wa zamani, Simba SC wamepangwa kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Mabao ya Simba leo yamefungwa na Nahodha John Raphael Bocco matatu dakika za nne, 18 na 69 na beki mkongwe, Shomari Kapombe dakika ya 36.
  Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 27 katika mchezo wa 12 na kurejea kileleni ikiwazidi pointi moja mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi mbili mkononi.
  Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao 11 za mechi 13 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: BOCCO APIGA HAT TRICK SIMBA YASHINDA 4-0 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top