• HABARI MPYA

  Tuesday, November 01, 2022

  DODOMA YAIVIMBIA POLISI ARUSHA, SARE 1-1


  TIMU ya Polisi Tanzania imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
  Kiungo Iddi Kipagwile alianza kuifungia Polisi Tanzania dakika ya 52, kabla ya Collins Opare kuisawazishia Dodoma Jiji FC dakika ya 90 na ushei, mabao yote yakipatikana kwa njia za penalti.
  Timu zote zinafikisha pointi sita baada ya sare hiyo, Dodoma Jiji katika mchezo wa tisa na inasogea nafasi y 15 na Polisi katika mchezo wa 10 na inasogea nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: DODOMA YAIVIMBIA POLISI ARUSHA, SARE 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top