• HABARI MPYA

  Wednesday, November 16, 2022

  GEITA GOLD YAWATANDIKA PRISONS 4-2 SOKOINE


  TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa ugenini wa 4-2 dhidi ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.
  Mabao ya Geita Gold yamefungwa na Yussuf Kagoma dakika ya 34, Daniel Lyanga dakika ya 45 na ushei, Shawn Oduro dakika ya 58 na Edmund John dakika ya 71, wakati ya Prisons yamefungwa na Oscar Paul Dalila ya 11 na Shawn Oduro aliyejifunga dakika ya 46.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 17 katika mchezo wa 12 na kusogea nafasi ya sita, wakati Prisons inabaki na pointi zake 14 za mechi 12 nafasi ya 10.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAWATANDIKA PRISONS 4-2 SOKOINE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top