• HABARI MPYA

  Friday, November 25, 2022

  GEITA GOLD YAICHAPA IHEFU 1-0 NA KUPANDA NNE BORA LIGI KUU


  TIMU ya Geita Gold imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara leo Uwanja wa Nyankumbu mjini Geita.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji Juma Luizio dakika ya 41 akimalizia pasi ya kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza.
  Kwa ushindi huo, Geita Gold inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 14 na kusogea nafasi ya nne, wakati Ihefu inabaki na pointi zake nane za mechi 13 sasa nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi ya timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: GEITA GOLD YAICHAPA IHEFU 1-0 NA KUPANDA NNE BORA LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top