• HABARI MPYA

    Wednesday, November 23, 2022

    CHOMOKA NA NDINGA MPYAA MSIMU HUU WA KOMBE LA DUNIA


    ZIKIWA zimepita siku chache tokea kuanza kwa michuano ya Kombe la Dunia huko nchini Qatar, K
    ampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch Tanzania imewapa wateja wake na wadau wote wa kubeti mchongo wa kujishindia gari mpya na ya kisasa kabisa, simu janja pamoja na bodaboda kutoka katika kampeni yao ya Chomoka na Ndinga.
    Hayo yamebainishwa na Afisa Habari wa Parimatch Tanzania, Ismael Mohamed wakati alipokuwa akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kampeni hiyo leo na kusema kuwa Promosheni hiyo ni mahususi kwa wateja wao wote wa Parimatch wenye akaunti na hata wateja wapya watakaojiunga katika kipindi hichi cha Kombe la Dunia.
     
    “Katika kipindi cha kuanzia 22.11.2022 hadi 26.12.2022, mteja wa Parimatch akifanya bashiri  kwenye mchezo wowote basi ataingia moja kwa moja katika droo wa kuwania Gari aina ya Urban Cruiser yenye O kilometa kutoka kwenye Showroom ya Toyota Tanzania, Bodaboda aina ya Hero Hunter  125cc na smartphone aina ya Samsung Galaxy A03 Core (Simu janja)”, alisema Ismael.
     
    Aidha Ismael aliendelea kwa kusema kuwa “Kila siku tutakuwa tunatoa simu mbili (2) na washindi watakuwa wanatangazwa kupitia kurasa zetu za kijamii na Zawadi ya Bodaboda itatolewa kwa wiki mara moja siku ya Ijumaa kupitia droo itakayoruka ITV wiki husika. Zawadi ya Gari itatolewa mwisho wa mashindano haya tarehe 27 Disemba ambapo droo kubwa ya kutafuta mshindi wa gari itafanyika siku hiyo”.
     
    Pamoja na hayo, Ismael amefafanua kuwa katika promosheni hiyo Sehemu ya michezo ya TVBET, Live Casino, Casino New na michezo ya Virtual haitaruhusiwi kushiriki katika promosheni hiyo.
    Kampuni ya Parimatch ndio kinara wa michezo ya kubashiri mtandaoni na imekuwa ikitoa ofa kubwa ya bonasi ya 100% mpaka TZs 1,000,000 kwa wateja wapya wanaojiunga nasi! Parimatch imekuwepo nchini Tanzania tangu mwaka 2019, ikitoa huduma nzuri ikijumuisha malipo ya haraka, odds kubwa na promosheni za kusisimua kwenye soka, Kasino na Michezo ya virtual. Mbali na soka, kampuni ya Parimatch pia hutoa mamia ya matukio kila siku kwenye tenisi, UFC, mpira wa vikapu, Kriketi, baseball na michezo mingine mingi ya Live na pre-match
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: CHOMOKA NA NDINGA MPYAA MSIMU HUU WA KOMBE LA DUNIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top