• HABARI MPYA

  Saturday, November 12, 2022

  SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 1-0 NA KUISHUSHIA YANGA NAFASI YA TATU


  BAO pekee la winga Msenegal, Pape Ousmane Sakho dakika ya 63 limeipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ihefu SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Simba was SC inafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya pili, ikizidiwa pointi mbili na vinara, Azam FC ambao pia wamecheza mechi moja zaidi.
  Mabingwa watetezi, Yanga wanashukia nafasi ya tatu sasa na pointi zao 20 za mechi nane, ingawa kesho unaweza kurejea kileleni kama itashinda dhidi ya Kagera Sugar Jijini Mwanza.
  Ihefu yenyewe baada ya kichapo cha leo hali inazidi kuwa mbaya, ikiendelea kushika mkia kwa pointi zake tano za mechi 10 sasa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAICHAPA IHEFU SC 1-0 NA KUISHUSHIA YANGA NAFASI YA TATU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top