• HABARI MPYA

  Sunday, November 06, 2022

  SIMBA QUEENS YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA


  TIMU ya Simba Queens jana imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Mabingwa Wanawake Afrika baada ya ushindi wa 2-0 dhidi ya Green Buffaloes ya Zambia jana Uwanja wa Marrakech Jijini Marrakech nchini Morocco.
  Mabao ya Simba Queens yalifungwa na Asha Djaffary dakika ya 64 na Opah Clement dakika ya 78 na kwa ushindi huo wanamaliza na pointi sita nyuma ya wenyeji, FAR Rabat waliomaliza  na pointi tisa.
  Rabat na Simba zote zinakwenda Nusu Fainali, huku Green Buffaloes iliyoambulia pointi tatu na Determine Girls ya Liberia iliyofungwa mechi zote zikirejea nyumbani.
  Simba itamenyana na kinara wa Kundi B katika Nusu Fainali Mamelodi, Sundowns na Rabat itacheza na washindi wa pili Bayelsa Queens ya Nigeria. 
  Kundi B Mamelodi imemaliza na pointi sita na Bayesla pointi tatu sawa timu na TP Mazembe ya DRC iliyomaliza ya tatu ikizidiwa ru wastani wa mabao, huku Wadi Degla ya Misri ikishika mkia baada ya kuoteza mechi zote tatu.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: SIMBA QUEENS YATINGA NUSU FAINALI LIGI YA MABINGWA AFRIKA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top