WENYEJI, Manchester City wamehitimisha mechi zao za Kundi G Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya Sevilla usiku wa jana Uwanja wa Etihad Jijini Manchester.
Mabao ya Man City yamefungwa na Rico Lewis dakika ya 52, Julian Álvarez dakika ya 73 na Riyad Mahrez dakika ya 83, baada ya Rafa Mir kuanza kuifungia Sevilla dakika ya 31.
Manchester City inamaliza mechi zake na pointi 14, mbele ya Borussia Dortmund pointi tisa, Sevilla pointi tano na FC Copenhagen pointi tatu.
0 comments:
Post a Comment