• HABARI MPYA

  Sunday, November 13, 2022

  KINDA CLEMENT AING’ARISHA YANGA KIRUMBA


  MABINGWA watetezi, Yanga SC wamerejea kileleni mwa Ligi Kuu ya Tanzania Bara baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Kagera Sugar Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza.
  Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, chipukizi Clement Mzize aliyepandishwa kutoka timu ya vijana dakika ya 19 akitumbukiza mpira nyavuni kwa kichwa cha mkizi kumalizia krosi ya kiungo Feisal Salum kutoka kulia.
  Shujaa mwingine wa pointi tatu za leo Yanga ni kipa wa Kimataifa wa Mali, Djigui Diarra aliyepangua mkwaju wa penalti wa Erick Mwijage baada ya yeye mwenyewe kumuangusha mshambuliaji mkongwe, Mganda Hamisi Kiiza ‘Diego’ kwenye boksi.
  Kwa matokeo hayo, Yanga inafikisha pointi 23 katika mchezo wa tisa na kurejea kileleni ikiizidi tu wastani wa mabao Azam FC ambayo pia imecheza mechi mbili zaidi.
  Baada ya kichapo cha leo, Kagera Sugar inabaki na pointi zake 11 za mechi 11 nafasi ya 13.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: KINDA CLEMENT AING’ARISHA YANGA KIRUMBA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top