• HABARI MPYA

  Monday, November 14, 2022

  MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 PALE PALE LONDON


  TIMU ya Manchester United jana iliibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya wenyeji, Fulham FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Craven Cottage Jijini London.
  Mabao ya Manchester United yalifungwa na C. Eriksen dakika ya 14 na A. Garnacho dakika ya 90 na ushei, wakati la Fulham lilifungwa na D. James dakika ya 61.
  Kwa ushindi huo, Manchester United wanafikisha pointi 26 katika mchezo wa 14, ingawa wanabaki nafasi ya tano wakizidiwa pointi tatu na Tottenham Hotspur ambayo pia imecheza mechi moja zaidi.
  Kwa upande wao, Fulham baada ya kichapo hicho wanabaki na pointi zao 19 za mechi 15 nafasi ya tisa.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAN UNITED YAICHAPA FULHAM 2-1 PALE PALE LONDON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top