• HABARI MPYA

  Tuesday, November 15, 2022

  AZAMFC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUIPIGA RUVU 1-0 CHAMAZI


  BAO la penalti la mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 73 limetosha kuipa Azam FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Kwa ushindi huo, Azam FC inafikisha pointi 26 katika mchezo wa 12 na kurejea kileleni mwa Ligi Kuu, ikiwazidi pointi tatu mabingwa watetezi, Yanga ambao wamecheza mechi tisa.
  Kwa upande wao, Ruvu Shooting wanabaki na pointi zao 11 za mechi 12 nafasi ya 13 kwenye ligi y timu 16.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAMFC YAREJEA KILELENI BAADA YA KUIPIGA RUVU 1-0 CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top