• HABARI MPYA

  Tuesday, November 22, 2022

  MAYELE APIGA MBILI YANGA YASHINDA 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU


  MABAO ya mshambuliaji Mkongo, Fiston Kalala Mayele dakika ya 42 na 67 yameipa Yanga SC ushindi wa 2-0 dhidi ya wenyeji, Dodoma Jiji FC Uwanja wa LITI mjini Singida.
  Mayele alifunga bao la kwanza akimalizia krosi ya Mkongo mwenzake, Tuisila Kisinda kutoka upande wa kulia na la pili akimalizia pasi ya winga chipukizi, Dennis Nkane.
  Mkongo huyo sasa anafikisha mabao manane na kupanda kileleni kwenye chati ya ufungaji kwa bao moja zaidi ya Sixtus Sabilo wa Mbeya City.
  Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi 29 katika mchezo wa 11 na kurejea kileleni ikiizidi wastani wa mabao tu Azam FC ambayo imecheza mbili zaidi.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MAYELE APIGA MBILI YANGA YASHINDA 2-0 NA KUREJEA KILELENI LIGI KUU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top