• HABARI MPYA

  Wednesday, November 09, 2022

  AZAM FC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 NA KUIFIKIA YANGA POINTI


  WENYEJI, Azam FC wameibuka na ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara usiku huu Uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
  Mabao ya Azam FC yamefungwa na kiungo mzawa, Ismail kader dakika ya 38 na mshambuliaji Mkongo, Idris Mbombo dakika ya 90 na ushei kwa pelnati, wakati la Dodoma Jiji FC limefungwa na mshambuliaji Mkenya, Collins Opare dakika ya 41.
  Kwa matokeo hayo, Azam FC inafikisha pointi 20 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya pili ikizidiwa tu wastani wa mabao na mabingwa watetezi, Yanga ambao wana mechi mbili mkononi, wakati Dodoma Jiji FC wanabaki na pointi zao sita za mechi 10 sasa nafasi ya 14.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AZAM FC YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 NA KUIFIKIA YANGA POINTI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top