• HABARI MPYA

  Friday, September 03, 2021

  COASTAL UNION YASAJILI WANIGERIA, MCAMEROON

   KIUNGO Mnigeria, Victor Patrick Akpan ni miongoni mwa wachezaji wapya waliosajiliwa na mabingwa wa zamani wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, Coastal Union ya Tanga.
  Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Wagosi wa Kaya kutoka JKU ya Zanzibar aliyojiunga nayo mwaka 2018.
  Wengine wapya waliosajiliwa Coastal Union ni mabeki wa kati Mkenya, Sosthenes Idah kutoka Bandari ya kwao, Joseph Zziwa kutoka Biashara United na kiungo Mcameroon Ngamchiya Amza kutoka Bamboutos ya kwao.
  Wengine ni wazawa makipa Mohammed Hussein kutoka Gwambina, Mussa Mbisa kutoka Mwadui FC, mabeki Yussuf Jamal, Amani Kyata kutoka Namungo FC na Mussa Said kutoka KMKM.


  Wapo pia viungo Hassan Sembi kutoka Stars of Africa ya Afrika Kusini, Gustapha Simon kutoka Gwambina, washambuliaji Jacob Benedicto, Edwin Charles, Vincent Abubakar kutoka DTB, Adam Uledi kutoka African Sports na James Ambroce kutoka Pamba.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YASAJILI WANIGERIA, MCAMEROON Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top