• HABARI MPYA

  Thursday, November 29, 2018

  NEYMAR AWAUA LIVERPOOL PARC DES PRINCES, WAFA 2-1 KWA PSG

  Neymar akishangilia baada ya kuifungia Paris Saint-Germain bao la ushindi dakika ya 37 ikiilaza Liverpool 2-1 katika mchezo wa Kundi C Ligi ya Mabingwa Ulaya usiku wa jana Uwanja wa Parc des Princes.
  Bao la kwanza la PSG lilifungwa na Juan Bernat dakika ya 13, wakati la Liverpool lilifungwa na James Milner dakika ya 45 na ushei kwa penalti baada ya Marco Verratti kumchezea rafu Joe Gomez.
  Kwa matokeo hayo, PSG inafikisha pointi nane ikiendelea kukamata nafasi ya pili, nyuma ya Napoli yenye pointi tisa baada ya jana kuifunga Crvena Zvezda 3-1, Liverpool inafuatia kwa pointi zake nne.
  Liverpool itahitaji ushindi kwenye mechi yake ya mwisho na Napoli wiki ijayo ili kujihakikishia kuingia hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo  
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: NEYMAR AWAUA LIVERPOOL PARC DES PRINCES, WAFA 2-1 KWA PSG Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top