• HABARI MPYA

  Friday, November 30, 2018

  MECHI ZA USIKU ZA LIGI KUU YA BARA ZARUHUSIWA KUCHEZWA UWANJA WA TAIFA BAADA YA KUSITISHWA GHAFLA JANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zilizokuwa zichezwe usiku kabla ya kurudishwa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitaendelea na ratiba ya awali kama inavyoonesha kwenye ratiba.
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba baada ya kushauriana/kujadiliana na mmiliki wa Uwanja wa Taifa, changamoto zilizosababisha mechi hizo za saa 12:00 jioni na saa 1:00 usiku kurudishwa saa 10:00 imeshughulikiwa na kumalizwa.
  Hivyo mechi zote zilizopo kwenye ratiba ya kuchezwa usiku zitaendelea kama zinavyoonesha kwenye ratiba.  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZA USIKU ZA LIGI KUU YA BARA ZARUHUSIWA KUCHEZWA UWANJA WA TAIFA BAADA YA KUSITISHWA GHAFLA JANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top