• HABARI MPYA

    Tuesday, November 20, 2018

    ALIYETULOGA MAREHEMU! BAO LA DAKIKA YA 89 LAITUPA NJE TANZANIA MBIO ZA OLIMPIKI YA 2020 JAPAN

    Na Mwandishi Wetu,  DAR ES SALAAM
    TIMU ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 23 imetupwa nje ya mbio za kuwania tiketi ya Olimpiki ya mwaka 2020 nchini Japan pamoja na ushindi wa 3-1 dhidi ya Burundi usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Burundi inaitoa Tanzania kwa faida ya bao la ugenini kuhesabika mara mbili baada ya ushindi wa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Alhamisi iliyopita mjini Bujumbura.
    Pamoja na matokto ya jumla kuwa 3-3, lakini Burundi inasonga mbele kwa bao lake la ugenini lililofungwa na Cedric Mavugo‬ ‪dakika ya 89.
    Mavugo aliyefunga pia dakika ya 79 katika ushindi wa 2-0 wa Burundi dhidi ya Tanzania Alhamisi iliyopita – alifunga bao hilo baada ya Tanzania kufanikiwa kuongoza kwa 3-0 kwa muda mrefu.

    Mabao ya Tanzania yamefungwa na Habib Hajji Kyombo dakika ya nne, Mbaraka Yussuf dakika ya 43 na Salum Kihimbwa dakika ya 70. 
    Na matokeo haya yanakuja siku mbili tu baada ya Tanzania kufungwa 1-0 na Lesotho mjini Maseru Jumapili katika mchezo wa Kundi L kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini Cameroon.
    Kipigo hicho kimepunguza matumaini ya Tanzania kufuzu AFCON, kwani Lesotho iliyofikisha pointi tano sawa na Taifa Stars inapanda nafasi ya pili nyuma ya Uganda iliyofuzu tayari kwa pointi zake 13 huku Cape Verde ikiwa inashika mkia kwa pointi zake nne.  
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALIYETULOGA MAREHEMU! BAO LA DAKIKA YA 89 LAITUPA NJE TANZANIA MBIO ZA OLIMPIKI YA 2020 JAPAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top