• HABARI MPYA

  Jumatatu, Novemba 26, 2018

  KUZIONA MTIBWA SUGAR NA NORTHEN DYNAMO SH. 2,000 TU KESHO UWANJA WA AZAM COMPLEX, CHAMAZI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, Mtibwa Sugar ya Morogoro wametaja viingilio vya mchezo wao wa kesho na Northern Dynamo.
  Mtibwa Sugar watakuwa wenyeji wa Northern Dynamo kesho katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Viingilio katika mchezo huo wa kwanza wa Raundi ya Awali Kombe la Shirikisho Afrikani Sh, 2,000 kwa majukwaa ya mzunguko na Sh. 3,000 kwa VIP.  

  Mchezo huo utachezeshwa na Waamuzi kutoka nchini Zimbabwe. Mwamuzi wa katikati Pilan NCUBE,Mwamuzi msaidizi namba moja Edgar Rumeck, mwamuzi msaidizi namba mbili Tafadzwa Nkala, Mwamuzi wa akiba Nomore Murambiwa Musundire, Kamisaa Gaspard Kayijuka wa Rwanda.
  Mchezo wa Simba dhidi ya Mbabane Swallows utachezwa Jumatano Novemba 28,2018 saa 10 jioni Uwanja wa Taifa.
  Mchezo huo utachezeshwa na Waamuzi kutoka Burundi. Mwamuzi wa katikati Pacifique NDABIHAWENIMANA,Mwamuzi msaidizi namba 1 Willy Habimana,Mwamuzi Msaidizi namba 2 Gustave Baguma,Mwamuzi wa akiba Georges Gatogato,Kamishna wa mchezo anatokea Zambia Joseph Nkole.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KUZIONA MTIBWA SUGAR NA NORTHEN DYNAMO SH. 2,000 TU KESHO UWANJA WA AZAM COMPLEX, CHAMAZI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top