• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 21, 2018

  EMMANUEL NZUKI WA MBEZI JUU AJINYAKULIA BAJAJI DROO YA 57 YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA NA KUSEMA…

  KUMEKUCHA Kwenye Promosheni ya Shinda Zaidi na SportPesa maana watanzania wanazidi kushinda bajaj kutokana na ubashiri wanaofanya kupitia timu ya ushindi.
  Safari hii kambi ya timu ya ushindi imehamia hapa jijini Dar es salaam katika viunga vya Mbezi Juu ambapo kuna mshindi wa droo ya 57 Emmanuel Nzuki anayekabidhiwa bajaj baada ya ushindi.
  Akizungumza baada ya kukabidhiwa bajaj hiyo Nzuki alisema hakuamini kama anaweza kushinda maana mara kadhaa alikuwa anacheza mara nyingi lakini hakubahatika kumbe wakati wake ulikuwa haujafika kubahatika sasa ndio ameamini baada ya kuupokea ushindi huo.
  Mshindi wa droo ya 57 ya Shinda Zaidi na SportPesa, Emmanuel Nzuki akiwa na bajaji yake baada ya kukabidhiwa 


  "Ama kweli nimeamini bahati ya mtu haipotei unajua vile nilikuwa nikiona wengine wakishinda nilijua labda wanaoshinda ni wale wenye kipato cha chini kabisa kumbe hata sisi wenye kipato cha kati inawezekana, siku ya leo yote naitumia kusherekea ushindi wangu" alisema Nzuki.
  Aidha mshindi huyo aliongeza kuwa bajaj hiyo itaweza msaidia kuinua kipato chake na kuacha maisha ya kutegemea mshahara pekee.
  "Sikia nikwambie aisee ni kweli nina mshahara mzuri lakini bado bajaj hii itakuwa msaada mkubwa kwangu maisha ya kutegemea mshahara pekee ni magumu sana lakini kupitia bajaj hii naweza sasa boresha maeneo mengine mfano kulipia watoto wangu ada ya shule kuwasaidia ndugu na pesa nyingine naweza malizia malipo ya kiwanja changu na kuanza kujenga.
  Mshindi huyo wa droo ya 57 aliwasisitiza watanzania kuacha woga na kujaribu bahati na SportPesa maana hata yeye wakati anaambiwa acheze hakuamini kama angeshinda lakini sasa tayari amefanikiwa kushinda na anamiliki bajaj yake aliyoshinda na SportPesa.
  Kwa upande wa SportPesa Meneja Uhusiano Bi Sabrina Msuya alisema prom0sheni yetu ni kwa mitandao yote ya simu na mteja anaweza kushiriki kupitia simu yake ya mkononi kwa kupiga * 150*87# na kuweka pesa kwenye akaunti yake ya SportPesa kupitia AirtelMoney, MPESA, TigoPesa na Halopesa kisha kuweka ubashiri wake.
  “Mbali na kushinda fedha za ubashiri wake ambazo huingizwa papo hapo kwenye akaunti ya mteja mara baada ya kubashiri kwa usahihi michezo aliyoweka, mteja anaweza kujishindia zawadi mbalimbali kama Bajaji, Simu janja(Smartphone), Jersey za Simba na Yanga pamoja na safari ya kwenda Hispania na Uingereza kushuhudia mitanange ya ligi zinazoendelea nchini humo”
  “Michezo anayoweza kushiriki ni pamoja na Jackpot (yenye mechi 13 ambayo kwa sasa ni zaidi ya shilingi milioni 394 yaani karibia milioni 400, hii ni Jackpotyenye kiasi kikubwa kuliko Jackpot zingine zozote nchini, pia mteja akibashiri kwa usahihi mechi kuanzia 10 hadi 12 anajipatia bonus kama zawadi”
  “Napenda kuwahamasisha watanzania wote kwamba washiriki na waendelee kubashiri na SportPesa kwani kuna mambo mbalimbali yanaendelea na wategemee mazuri zaidi kutoka kwetu”.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: EMMANUEL NZUKI WA MBEZI JUU AJINYAKULIA BAJAJI DROO YA 57 YA SHINDA ZAIDI NA SPORTPESA NA KUSEMA… Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top