• HABARI MPYA

  Monday, November 26, 2018

  RAJA YAITANDIKA AS VITA 3-0 FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

  TIMU ya Raja Casablanca jana imetumia vyema Uwanja wa nyumbaji, Mohamed V mjini Casablanca baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika fainali ya kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Pongezi kwa mshambuliaji kinda Mmorocoo mwenye umri wa miaka 22, Soufiane Rahimi aliyefunga mabao mawili jana na kuisogeza timu yake karibu na taji hilo la pili kwa ukubwa katika michuano ya klabu barani.
  Rahimi alifunga mabao yote kwa pasi mshambuliaji pacha wake, Mahmoud Benhalib mwenye umri wa miaka 22 pia dakika za 47 na 61.

  Rahimi angeweza kufunga hat tric jana angekimbilia penalti iliyoipa Raja bao la tatu dakika ya 66, lakini akamuachia pacha wake, Benhalib aiweke timu hiyo kwenye nafasi nzuri kuelekea mchezo wa marudiano.
  Kwa matokeo hayo, AS Vita sasa inatakiwa kwenda kushinda 4-0 nyumbani Desemba 2 Uwanja wa Martyrs de la Pentecote mjini Kinshasa ili kupindua matokeo na kubeba taji hilo.
  AS Vita iliifunga 4-0 Al - Masry ya Misri Oktoba 24 katika mchezo wa marudiano wa Nusu Fainali ya michuano, lakini ikitoka kutoa sare ya 0-0 ugenini.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: RAJA YAITANDIKA AS VITA 3-0 FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top