• HABARI MPYA

  Friday, November 30, 2018

  ARSENAL YAFUZU HATUA YA MTOANO EUROPA LEAGUE

  Wachezaji wa Arsenal, Mohamed Elneny (kushoto) na Emile Smith Rowe (kulia) wakimpongeza kinda Muingereza mwenye umri wa miaka 19, Joe Willock baada ya kuifungia timu hiyo bao la tatu dakika ya 41 katika ushindi wa 3-0 dhidi ya wenyeji, Vorskla kwenye mchezo wa Kundi E Europa League usiku wa jana Uwanja wa NSK Olimpiki mjini Kiev. 
  Mabao mengine ya The Gunners yalifungwa na  Emile Smith Rowe dakika ya 10 na Aaron Ramsey kwa penalti dakika ya 27 na kwa ushindi huo, Arsenal inafikisha pointi 13 kuelekea mechi za mwisho ikifuzu hatua ya mtoano kwa pamoja na Sporting Lisbon yenye pointi 10, wakizipiku Vorskla na Qarabag zenye pointi tatu kila moja 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ARSENAL YAFUZU HATUA YA MTOANO EUROPA LEAGUE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top