• HABARI MPYA

  Monday, November 19, 2018

  MGAYA HASSAN, MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU MOROGORO AJISHINDIA BAJAJI YA SPORTPESA KATIKA DROO YA 43

  TANGU ameanza kucheza SportPesa haikuchukua muda mrefu mpaka pale alipotangazwa kuwa ni mshindi wa Shinda Zaidi na SportPesa na kufanikiwa kushinda bajaj mpya kabisa kutoka timu ya ushindi 
  Huyu ni Mgaya Hassan mshindi wa Droo Ya 43 yeye ni mwanafunzi wa chuo kikuu na mkoani Morogoro lakini ushindi wa bajaj umemkuta akiwa hapa jijini Dar es Salaam wakati akimalizia likizo yake kwa kaka yake.
  Na Timu Ya Ushindi haikutaka Kumcheleweshea Ilimfuata mpaka Bunju Hapa Dar es Salaam Nyumbani kwa Kaka Yake Na Kumkabidhi Bajaj.
  Akikabidhiwa bajaji ya ushindi Hassan alisema alianza kucheza na SportPesa baada ya kusikia kwenye redio na tv kuwa kuna bajaj zinatolewa na yeye moja kwa moja akijasajili na kuanza kutupia bashiri kwenye mechi  mbalimbali hatimaye kufanikiwa kushinda.

  Mgaya Hassan akiwa na fungo yake baada ya kukabidhiwa kufuatia kushinda droo ya 43

  "Mimi ni mwanafunzi nasoma SUA Morogoro taarifa hizi za ushindi zimenikuta hapa Dar es salaam wakati nikiwa likizo, nimefurahi sana maana wakati nacheza wanafunzi wenzangu waliniambia mimi siwezi kushinda kwa sababu naweka pesa ndongondogo waliamini kuwa wanaoshinda ni wale ambao hubashiri kwa pesa nyingi kumbe sivyo kila mtu ana nafasi ya kushinda maana mimi nilikuwa nacheza kwa elfu moja moja pekee sasa nimeshinda najua  wakiniona ndio wataamini yani nina furaha sana" alisema Hassan
  Aidha Hassan anasema bajaji hii itamkomboa kutoka kwenye maisha ya sintofahamu na kuingia kwenye maisha mazuri huku akitegemea kipato kitakachopatikana kutokana na bajaj kumsaidia kwenye mahitaji yake ya chuoni na nyingine kuwawezesha ndugu zake ambao hawako vizuri kiuchumi.
  "Daaah maisha ya chuo ni magumu sana unatoka chuo umechoka wakati mwingine huna pesa ya kula familia zetu nazo zinatoka katika mazingira ya kimaskini unajikuta huna cha kufanya lakini kwa ushindi huu wa bajaj ntaweza jikimu mimi mwenyewe maana kila siku ntakuwa na uhakika wa kupata chochote kutokana na bajaji hii" aliongeza Hassan.
  Hassan aliwaomba wanafunzi wenzake wa vyuoni wale ambao wamefikisha umri wa miaka 18 na zaidi kucheza na SportPesa maana wanaweza  jikuta wakiandika historia mpya kwenye maisha yao na kumudu gharama  ndogondogo zinazopatikana chuoni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MGAYA HASSAN, MWANAFUNZI WA CHUO KIKUU MOROGORO AJISHINDIA BAJAJI YA SPORTPESA KATIKA DROO YA 43 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top