• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 28, 2018

  BOMU LALIPULIWA UWANJANI MECHI YA LIGI YA MABINGWA UGIRIKI

  Bomu la Petroli lililolipuliwa na mashabiki wa AEK Athens jukwaani Uwanja wa Olympiako Spyros Louis mjini Athens, Ugiriki katika mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Ajax usiku wa jana.
  Vurugu kubwa ziliibuka mashabiki wa AEK Athens waliwashambulia na kuwajeruhi mashabiki wa Ajax, ingawa Polisi walifanikiwa kutuliza vurumai hizo na mechi ikachezwa wageni wakiibuka na ushindi wa 2-0, mabao ya mshambuliaji Mserbia, Dusan Tadic dakika za 68 na 72.
  Ajax imemaliza nafasi ya pili kwenye kundi hilo kwa pointi zake 11, nyuma ya Bayern Munich iliyomaliza na pointi 13 na zote zote zinakwenda hatua ya 16 Bora Ligi ya Mabingwa Ulaya zikizipiku Benfica iliyomaliza na pointi nne na AEK Athens iliyotoka kapa 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: BOMU LALIPULIWA UWANJANI MECHI YA LIGI YA MABINGWA UGIRIKI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top