• HABARI MPYA

  Alhamisi, Novemba 29, 2018

  UCHAGUZI MDOGO WA BARAZA KUU BODI YA LIGI KUFANYIKA KESHOKUTWA MGOMBEA PEKEE UENYEKITI MNGUTO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MKUTANO wa Baraza Kuu la Bodi ya Ligi (TPLB) unatarajia kufanyika keshokutwa, Jumamosi ya Desemba 1, mwaka huu mjini Tanga. 
  Mkutano huo utafanyika kwenye hotel ya Regal Naivera saa 3 asubuhi.
  Aidha Mkutano huo utatumika kujaza nafasi zilizo wazi za Mwenyekiti na Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Kwanza na Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Pili.
  Mwenyekiti wa Coastal Union ya Tanga, Steven Mnguto ndiye mgombea pekee anayegombea nafasi ya Mwenyekiti wakati Azim Khan na Brown Ernest wakigombea nafasi ya Mjumbe anayewakilisha klabu Ligi Daraja la Kwanza na Michael Kadebe yeye akigombea nafasi ya kuwakilisha klabu Ligi Daraja la Pili.
  Steven Mnguto (kulia) ndiye mgombea pekee wa nafasi ya Uenyekiti wa Bodi ya Ligi 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: UCHAGUZI MDOGO WA BARAZA KUU BODI YA LIGI KUFANYIKA KESHOKUTWA MGOMBEA PEKEE UENYEKITI MNGUTO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top