• HABARI MPYA

  Jumapili, Novemba 18, 2018

  ENGLAND WAICHAPA CROATIA 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI

  Wachezaji wa England, Harry Kane na Jesse Lingard wakiwa wamelaliana kwa furaha baada ya wote kuifungia Three Lions katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Croatia kwenye mchezo wa Kundi la Nne Ligi ya Mataifa ya Ulaya usiku wa leo Uwanja wa Wembley mjini London. Lingard alifunga dakika ya 78 na Kane dakika ya 85, baada ya Andrej Kramaric kuanza kuifungia Croatia dakika ya 57 na kwa matokeo hayo, England inatinga Nusu Fainali ikifikisha pointi saba baada ya kucheza mechi nne, ikishinda mbili, sare moja na kufungwa moja.
  Inafuatiwa na Hispania yenye pointi sita baada ya kushinda mechi mbili na kufungwa mbili, wakati Croatia yenye pointi nne baada ya kushinda mechi moja, sare moja na kufungwa mbili inashika mkia 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: ENGLAND WAICHAPA CROATIA 2-1 NA KUTINGA NUSU FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top