• HABARI MPYA

  Wednesday, November 28, 2018

  ROBBEN, LEWANDOWSKI WAPIGA MBILI MBILI BAYERN YASHINDA 5-1

  Arjen Robben akishangilia baada ya kuifungia Bayern Munich bao la kwanza dakika ya 13 kabla ya kufunga na la pili dakika ya 30 katika ushindi wa 5-1 dhidi ya Benfica usiku wa jana kwenye mchezo wa Kundi E Ligi ya Mabingwa Ulaya Uwanja wa Allianz Arena mjini Munich. 
  Mabao mengine ya Bayern Munich yalifungwa na Robert Lewandowski mawili pia dakika za 36 na 51 na Franck Ribery dakika ya 76 wakati la Benfica lilifungwa na Gedson Fernandes dakika ya 46.
  Kwa ushindi huo, Bayern Munich inafikisha pointi 13 na kumalizia kileleni mwa Kundi E, ikifuatiwa na Ajax iliyomaliza na pointi 11 na zote zinafuzu hatua ya 16 Bora zikizipiku Benfica iliyomaliza na pointi nne na AEK Athens iliyofungwa mechi zote 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: ROBBEN, LEWANDOWSKI WAPIGA MBILI MBILI BAYERN YASHINDA 5-1 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top