• HABARI MPYA

  Jumatano, Novemba 28, 2018

  JKU WATANDIKWA 4-0 NA AL HILAL SUDAN LIGI YA MABINGWA, LEO ZIMAMOTO WANAMENYANA NA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, upande wa pili wa Jamhuri yetu ya Muungano, JKU usiku wa jana walichapwa  mabao 4-0 na Al Hilal Omdurman katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman.
  Mabao ya Al Hilal usiku wa jana yalifungwa na Mbrazil Geovane, Bunker Diarra kutoka Mali, Mkongo Mbombona Nahodha, Abdullateef Saeed.
  JKU wanarejea kinyonge sasa wakitakiwa kushinda 5-0 kwenye mchezo wa marudiano Desemba 4 ili kwenda raundi ya kwanza.
  Matokeo hayo yalikuja saa chache, baada ya wawakilishi wengine wa Tanzania, upande wa kwanza wa Muungano, Tanzania Bara kuanza vyema kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Northen Dynamo ya Shelisheli Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.

  Ushindi huo ulitokana na mabao ya washambuliaji Jaffar Salum Kibaya aliyefunga matatu na linguine mgtokea benchi Riffat Khamis Msuya na sasa Mtibwa Sugar watakuwa na kazi nyepesi kwenye mchezo wa marudiano wiki ijayo nchini Shelisheli.
  Wawakilishi wengine wa Tanzania Bara katika Ligi ya Mabingwa, Simba SC wanatarajiwa kumenyana na Mbabane Swallows ya Eswatini, zamani Swaziland katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali pia, kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Wawakilishi wengine wa Zanzibar kwenye Kombe la Shirikisho, Zimamoto leo watakuwa wageni wa Kaizer Chiefs Uwanja wa Nelson Mandela Bay mjini Port Elizabeth kuanzia Saa 2: 30 usiku.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: JKU WATANDIKWA 4-0 NA AL HILAL SUDAN LIGI YA MABINGWA, LEO ZIMAMOTO WANAMENYANA NA KAIZER CHIEFS AFRIKA KUSINI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top