• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 30, 2018

  SIMBA SC YAONDOKA KESHO KUIFUATA MBABANE SWALLOWS KWA MCHEZO WA MARUDIANO DESEMBA 4 BAADA YA KUMSAINI COULIBALY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Eswatini, zamani Swaziland kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wao wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mbabane Swallows, utakaochezwa Desemba 4 mwaka huu.
  Simba wanakwenda Swaziland na mtaji wabao 4-1 walioshinda kwenye mchezo wa kwanza Jumatano Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Ofisa habari wa klabu hiyo Haji Manara alisema kuwa kocha wao Mbelgiji Patrick Aussems, alisema kuwa wanaenda nchini humu kwa ajili ya kumalizia dakika 90 za pili.
  Alisema kuwa tayari wameshamaliza vyema  dakika 90 za kwanza na sasa wanaenda kwa kazi moja tu ya kumalizia  dakika 90 zijazo wakiwa kwao.
  Kocha Patrick J Aussems (kulia) kwa pamoja na Mtendaji Mkuu wa klabu, Crescentius Magori wakimkabidhi Zana Coulibaly Oumar jezi ya Simba
  Zana Coulibaly Oumar akifurahia na jezi yake ya Simba SC na chini ni wakati anasaini mkataba

  Alisema kuwa plani ya mwalimu ni kuhakikisha wanashinda raundi hii ya awali na kuingia hatua nyingine ili waweze kufikia malengo yao kucheza hatua za makundi.
  "Kocha anachokiitaji ni kuhakikisha timu yake inafika mbali zaidi  kwenye mashindano haya ndio maana anatengeneza kikosi na kuangalia mapungufu yaliokuwepo kwenye kikosi chake anayafanyia marekebisho ili waweze kwenda kupata ushindi huko kwao.
  Mwalimu wao anajua tabu za mechi za ugenini zinavyokuwa ngumu lakini kutokana na matokeo mazuri aliyoyapata hapa atahakikisha wanashinda na kusonga mbele," alisema Manara.
  Manara alisema kuwa utaondoka msafara wa watu 30, wakiwemo wachezaji 21,  benchi la ufundi pamoja na viongozi.
  Lakini pia alisema kuwa kunandege  ya Ethiopia ambayo itabeba mashabiki ambao watalipia dola za kimarekani 300 hadi Afrika kusini na baada ya hapo kama mashabiki watakuwa wengi basi watakodisha gari kutoka Afrika Kusini hadi Swaziland  kwa dola za kimarekani 50.
  Katika hatua nyingine, Manara alisema kuwa  hadi sasa mwalimu hajapendekeza jina la mchezaji wowote wa ndani kusajili wa zaidi ya beki wao mpya aliyetokea Asec Mimosas ya Ivory Coast, Zana Coulibaly Oumar.
  Alisema kuwa mwalimu alipendekeza asajiliwe mchezaji huyo kutokana na kumjua vizuri na  atawasaidia zaidi hasa kwenye michuano hii ya klabu bingwa.
  Nyota huyo wa Ivory Coast amesaini mkataba wa miaka miwili leo kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo.
  Hata hivyo Manara aliweka wazi hali ya beki wao Shomari Kapombe na kusema bado na anaendelea na matibabu yake nchini Afrika Kusini akihudumiwa na jopo la  madaktari wa nchini hapo kuhakikisha anapona kwa haraka.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: SIMBA SC YAONDOKA KESHO KUIFUATA MBABANE SWALLOWS KWA MCHEZO WA MARUDIANO DESEMBA 4 BAADA YA KUMSAINI COULIBALY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top