• HABARI MPYA

  Monday, November 26, 2018

  COASTAL UNION YAMREJESHA BEKI WAKE WA ZAMANI WA KULIA, MIRAJ ADAM ALIYEKIMBIA ‘NJAA’ SINGIDA UNITED

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  BEKI wa kulia, Miraj Adam amerejea katika klabu yake, Coastal Union ya Tanga baada ya kusaini mkataba wa miezi sita.
  Miraj aliyewahi kuchezea pia African Lyon ya Dar es Salaam, amesaini mkataba huo wa miezi sita kama mchezaji huru baada ya kuachana na klabu ya Singida United hivi karibuni.
  Adam aliachana na Singida United inayocheza Ligi Kuu ya Tanzania Bara kwa msimu wa pili tangu irejee, akidai hajalipwa mishahara na stahiki zake nyingine kwa muda mrefu.  

  Miraj Adam aliondoka Singida United baada ya kung'ara michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya katikati ya mwaka huu


  Miraj Adam alipokuwa Coastal Union (kushoto) akimdhibiti aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Donald Ngoma (kulia)
  Miraj Adam alipokuwa Singida United akimkimbilia aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga, Mzambia Obrey Chirwa  
  Miraj Adam alipokuwa African Lyon akijaribu kuondoa mpira miguuni mwa aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajib ambaye waliibuka naye timu ya vijana ya Wekundu hao wa Msimbazi
  Hapa Miraj Adam alipokuwa SImba SC akiondoka na mpira Uwanja wa Taifa
  Miraj Adam amerejea Coastal Union
  Mchezaji huyo wa Morogoro, aliibukia katika timu ya vijana ya Simba mwaka 2012 kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa ambako alicheza kwa misimu miwili hadi alipoachwa.
  Miraj amekuwa mchezaji wa timu za taifa za vijana kuanzia chini ya umri wa miaka 17 (U17), U20 na U23 na kuna wakati aliitwa pia timu ya wakubwa.
  Maumivu ya mguu msimu uliopita yalimrudisha nyuma mchezaji huyo kabla ya kupona na kurejea mwishoni mwa msimu na kwenda kung’ara kwenye michuano ya SportPesa Super Cup nchini Kenya, lakini matatizo ya kiuchumi yanayoikabili klabu hiyo yamemkimbiza. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: COASTAL UNION YAMREJESHA BEKI WAKE WA ZAMANI WA KULIA, MIRAJ ADAM ALIYEKIMBIA ‘NJAA’ SINGIDA UNITED Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top