• HABARI MPYA

  Thursday, November 29, 2018

  WAWAKILISHI WOTE WA ZANZIBAR TAABANI MICHUANO YA AFRIKA, WAGONGWA ‘NNE NNE’ SASA WANATAKIWA KUSHINDA 5-0 NYUMBANI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika, Zimamoto kutoka upande wa pili wa Muungano, Zanzibar jana usiku wamechapwa mabao 4-0 na wenyeji, Kaizer Chiefs katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Uwanja wa Nelson Mandela mjini Port Elizabeth.
  Kipigo hicho imetokana na mabao ya Khama Billiat aliyefunga matatu peke yake dakika za saba, 60 na 73 wakati linguine likifungwa na Kabelo Mahlasela dakika ya 68.
  Zimamoto sasa wanakabiliwa na mtihani wa kuja kushinda 5-0 nyumbani katika mchezo wa marudiano Desemba 5 ili kusonga mbele. 
  Adhabu kama hiyo inawakabili wawakilishi wengine wa Zanzibar, JKU katika mchezo wa marudiano Desemba 4 baada ya juzi usiku kufungwa 4-0 na Al Hilal Omdurman katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Al-Hilal mjini Omdurman.

  Mchezaji wa Zimamoto (kulia) akimiliki mpira dhidi ya mchezaji wa Kaizer Chiefs jana Uwanja wa Mandela Bay
  Mchezaji wa Zimamoto akifungishwa tela na mchezaji wa Kaizer Chiefs jana  
  Mshambuliaji wa Kaizer Chiefs, Khama Billiat (katikati) akishangilia na wachezaji wenzake, Lebogang Manyama (kushoto) na Siphosakhe Ntiya-Ntiya baada ya kuwapiha hat trick Zimamoto FC 

  Mambo ni mazuri kwa wawakilishi wa Tanzania, baada ya timu zake zote, Simba SC na Mtibwa Sugar kuanza vyema mechi za kwanza za Raundi ya Awali kwa ushindi wa mabao manne nyumbani.
  Walianza Mtibwa Sugar kushinda 4-0 dhidi ya Northen Dynamo ya Shelisheli katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Komnbe la Shirikisho Afrika, mabao ya washambuliaji Jaffar Salum Kibaya aliyefunga matatu na lingine mtokea benchi Riffat Khamis Msuya.
  Wakafuatia Simba SC jana kushinda 4-1 kwenye mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali dhidi ya Mbabane Swallows ya Eswatini, zamani Swaziland Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Ushindi huo ulitokana na mabao mawili ya Nahodha John Bocco na wageni Meddie Kagere na Clatous Chama, unamaanisha Simba SC kama Mtibwa, imerahisisha kazi kuelekea mchezo wa marudiano Desemba 4 nchini Swaziland, kwani wenyeji watatakiwa kushinda 3-0 ili kusonga mbele.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: WAWAKILISHI WOTE WA ZANZIBAR TAABANI MICHUANO YA AFRIKA, WAGONGWA ‘NNE NNE’ SASA WANATAKIWA KUSHINDA 5-0 NYUMBANI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top