• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2018

  KIINGILIO RAHISI ZAIDI MECHI YA SIMBA NA MBABANE SWALLOWS LIGI YA MABINGWA AFRIKA KESHO NI SH 5,000 TAIFA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  KLABU ya Simba imetaja viingilio katika mchezo wake wa kesho na Mbabane Swallows ya Eswatini, zamani Swaziland utakaofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
  Simba SC wanawaalika Mbabane Swallows kesho Saa 10:00 jioni katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika ambao utaonyeshwa moja kwa moja na chaneli ya Azam Sports 2 ya Azam TV.
  Na jana Ofisa Habari wa klabu hiyo bingwa Tanzania Bara, Hajji Sunday Manara alisema kwamba kiingilio cha chini katika mchezo huo kitakuwa ni Sh. 5,000 kwa majukwaa ya mzunguko.
  Viingilio vingine alivyotaja Hajji ni Sh. 7,000 kwa eneo la VIP C, 10,000 eneo la VIP B na 20,000 kwa watakaoketi VIP A.
  Jitokezeni kwa wingi kesho mkaupendeshe Uwanja na kuishangilia kwa nguvu Simba yenu ishinde

  Manara alisema kwamba maandalizi ya mchezo yalikuwa mazuri na kwa ujumla kikosi tayari cha Simba SC kipo tayari kwa mchezo huo.
  “Tunakwenda kuwakabili Mbabane Jumatano tukijua ni timu nzuri na mabingwa wenzetu, lakini tunajua matarajio ya Watanzania na wana Simba kwetu. Kwa kweli hatutawaangusha na tunaahidi furaha kwenu,”amesema Manara. 
  Simba SC imepania kufika mbali msimu huu katika michuano ya Afrika baada ya msimu uliopita kutolewa katika Raundi ya Kwanza tu na Al Masry ya Misri kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
  Na ikiwa chini ya kocha mpya, Mbelgiji Patrick Aussems – Simba SC inaonyesha inaweza kutimiza dhamira yake, kwani kwa sasa inacheza soka ya kuvutia.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KIINGILIO RAHISI ZAIDI MECHI YA SIMBA NA MBABANE SWALLOWS LIGI YA MABINGWA AFRIKA KESHO NI SH 5,000 TAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top