• HABARI MPYA

  Jumanne, Novemba 27, 2018

  MTIBWA SUGAR YAANZA VYEMA MICHUANO YA AFRIKA, YAWATANDIKA WASHELISHELI 4-0 JAFFAR KIBAYA APIGA HAT TRICK

  Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM 
  TIMU ya Mtibwa Sugar ya Morogoro imeanza vyema michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Northern Dynamo ya Shelisheli jioni ya leo katika mchezo wa kwanza wa Raundi ya Awali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam.
  Shujaa wa Mtibwa Sugar leo alikuwa ni mshambuliaji Jaffar Salum Kibaya aliyefunga mabao matatu, huku bao la nne likifungwa mtokea benchi Riffat Khamis Msuya.
  Kibaya aliifungia Mtibwa Sugar bao la kwanza dakika ya 12 kwa shuti kali akimalizia pasi ya kiungo Salum Kihimbwa kabla ya kufunga la pili dakika 34 kwa shuti la umbali wa mita 17 baada ya kuwatoka mabeki wa Northen Dynamo.
  Wachezaji wa Mtibwa Sugar wakimpongeza Jaffar Kibaya baada ya kufunga bao la pili kati ya matatu leo Uwanja wa Azam Complex
  Beki wa Mtibwa Sugar, Ally Shomary akimtoka mchezaji wa Northen Dynamo, Darren Gonzales 
  Beki wa Mtibwa Sugar, Dickson Daudi akiwa ameruka dhidi ya mchezaji wa Northen Dynamo, Musa Njie 
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilichoanza leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam 
  Kikosi cha Northern Dynamo kilichoanza leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi mjini Dar es Salaam

  Kibaya akakamilisha hat trick yake dakika ya 57 kwa bao la mkwaju wa penalti baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye boksi na mabeki wa Northen Dynamo.
  Mshambuliaji chipukizi, Riffat Khamis Msuya aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Juma Luizio akaifungia bao la nne Mtibwa Sugar dakika ya 90.
  Na sasa Mtibwa Sugar inayofundishwa na mchezaji wake wa zamani, Zuberi Katwila itahitaji kwenda kuulinda ushindi wake mnono kwenye mchezo wa marudiano Desemba 4 nchini Shelisheli.
  Kikosi cha Mtibwa Sugar kilikuwa; Shaaban Kado, Ally Shomari, Issa Rashid ‘Baba Ubaya’, Cassian Ponera, Dickson Daudi, Shaaban Nditi, Salum Kihimbwa, Ismail Mhesa/Haruna Chanongo dk74, Jaffar Kibaya, Juma Liuzio/Riffat Msuya dk60 na Ally Makarani.
  Northen Dynamo; Ricky Pool/Francois Bodombo dk43, Esther Wesley, Rakotondrasoa Tolotra, Musa Njie, Kevin Estico, Stan Esther, Dufrene Aldo Samuel, Marcus Maria/Kevin Mirabeau dk71, Francis Moumou na Kieren Sinon.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: MTIBWA SUGAR YAANZA VYEMA MICHUANO YA AFRIKA, YAWATANDIKA WASHELISHELI 4-0 JAFFAR KIBAYA APIGA HAT TRICK Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top