• HABARI MPYA

  Ijumaa, Novemba 16, 2018

  TFF YASISTIZA HAITAMBUI UENYEKITI WA MANJI YANGA SC NA KAMA ANATAKA ACHUKUE FOMU AGOMBEE KWENYE UCHAGUZI WA JANUARI 13

  Na Nasra Omary, DAR ES SALAAM
  MWENYEKITI wa kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la  Soka Tanzania (TFF), Malangwe Mchungahela amesema kwamba hawamtambui Yussuf Manji kama  Mwenyekiti wa Yanga.
  Hayo yamekuja mara baada ya wajumbe wa kamati  ya utendaji walipokutana na mwenyekiti huyo huku  wakiwa na hoja ya kukubali kufanya uchaguzi  isipokuwa nafasi ya uwenyekiti.
  Mchungaha alisema kuwa kwa mujibu wa katiba ya  Yanga, ibara ya 28 kanuni ya tatu (c) inasema mjumbe  atakoma kuwa mjumbe wa kamati ya utendaji iwapo  atashindwa kutekeleza majukumu ya mjumbe  kutokana na kuumwa au sababu nyingine yoyote kwa  kipindi cha miezi 12 mfululizo.

  TFF Imesema haItambui Uenyekiti wa Yussuf Manji Yanga SC na akitaka kuendelea kuwa kiongozi wa klabu hiyo agombee

  Katiba hiyo ya marekebisho ya mwaka 2010, ibara ya  14 inamruhusu mwanachama yoyote kujiuzulu na  kuwasilisha barua kwa katibu mkuu wa Yanga kwa barua ya rejesta.
  Mchungahela alisema kuwa hawamtambui Manji  kama mwenyekiti wa Yanga kama katiba yao  inavyojieleza.
  Alisema kuwa kama Manji bado anahitaji nafasi ya  uenyekiti basi aende kuchukua fomu kabla mchakato  haujafungwa aili aweze kugombea tena.
  "Sisi kama TFF hatumtambui Manji kama mwenyekiti  wa Yanga maana alishakutana na Waziri wa Michezo,  Dk Harrison Mwakyembe ili kuzungumzia suala la  kurudi Yanga na alimkatalia.
  Lakini pia aliandikiwa barua na TFF ambao walitaka  kujua kama yeye bado mwenyekiti au la pia nayo  alikaidi kujibu na alikuuja kujibu majibu ambayo  hatoshelezi kujua kama yeye bado yupo kwenye  nafasi yake," alisema Mchungahela.
  Kwenye mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo  waliokutana Juni 10 mwaka huu kwenye Ukumbi wa  Maofisa wa Polisi, Oysterbay kwa pamoja walisema  wanamtambua Manji kama mwenyekiti wao na  wanamuamba amalizie miaka miwili iliyobaki  kwakuwa muda wake unatarajiwa kumalizika Juni  2020.
  Mei 23, mwaka jana Manji aliwasilisha barua ya  kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga,  Boniface Mkwasa, akidai kuwa anatoa nafasi kwa  wanachama wengine kuingoza klabu hiyo.
  Kwa muda ambao Manji alitangaza kujiuzulu mpaka  sasa kafikisha miezi 18 ambapo kapoteza sifa ya kuwa  mwanachama hai wa klabu hiyo.
  Mbali na Manji, wengine waliojiuzulu ni Clement  Sanga (makamu mwenyekiti), Salum Mkemi, Ayoub  Nyenzi, Said Ameir na Hashim Abdallah (wajumbe). 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: TFF YASISTIZA HAITAMBUI UENYEKITI WA MANJI YANGA SC NA KAMA ANATAKA ACHUKUE FOMU AGOMBEE KWENYE UCHAGUZI WA JANUARI 13 Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top