• HABARI MPYA

  Friday, November 30, 2018

  AFISA WA TANZANIA, LINA KESSY ATEULIWA KUSIMAMIA FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE KESHO GHANA

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MWANAMAMA wa Kitanzania, Lina Kessy (pichani kulia) ameteuliwa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kusimamia mchezo wa Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa Wanawake nchini Ghana. 
  Afisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Cliford Mario Ndimbo amesema kwamba Lina atakuwa Kamisaa wa mchezo huo wa Fainali utakaochezwa kesho Disemba 1, 2018 utakaowakutanisha Nigeria dhidi ya Afrika Kusini. 
  Mchezo huo namba 16 utachezwa Accra Sports mjini Accra kuanzia  Saa 10:00 jioni na itachezeshwa na mwamuzi kutoka Zambia Glady Lengwe atakayesaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 kutoka Madagascar Lidwine Rakotozafinoro, Mwamuzi msaidizi namba 2 Bernadettar Kwimbira kutoka Malawi na Mwamuzi wa akiba Fatou Thioune.
  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunamtakia kila la heri Lina Kessy tunaamini uwezo wake wa kusimamia michezo mikubwa kama huo wa Fainali ya Afrika kwa Wanawake. 

  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: AFISA WA TANZANIA, LINA KESSY ATEULIWA KUSIMAMIA FAINALI YA KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA KWA WANAWAKE KESHO GHANA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top