• HABARI MPYA

  Thursday, November 29, 2018

  MECHI ZOTE ZA LIGI KUU ZINAZOFANYIKA UWANJA WA TAIFA KUCHEZWA KUANZIA SAA 10:00 JIONI

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  MECHI zote za Ligi Kuu Tanzania Bara zitakazochezwa kwenye Uwanja wa Taifa,Dar es Salaam zitachezwa saa 10 jioni. 
  Awali kulikuwa kuna mechi zilizopangwa kuchezwa saa 12 jioni na saa 1 usiku. 
  Mechi zilizopangwa kuchezwa katika muda huo zimerudishwa saa 10 jioni kufuatia mmiliki wa Uwanja wa Taifa kutoa taarifa za kutowashwa taa za Uwanja ambazo zingehitajika kwa mechi hizo za jioni. 
  Utekelezaji wa taarifa hiyo ya wamiliki wa Uwanja inaanza kutekelezwa leo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Yanga SC vs JKT Tanzania mchezo ambao awali ulikuwa uchezwe saa 12 jioni.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 comments:

  Item Reviewed: MECHI ZOTE ZA LIGI KUU ZINAZOFANYIKA UWANJA WA TAIFA KUCHEZWA KUANZIA SAA 10:00 JIONI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top