• HABARI MPYA

    Monday, July 09, 2018

    KOCHA MASOUD JUMA AMSIFU KIUNGO MPYA MKONGO, ASEMA ATAISAIDIA SIMBA KUFANYA VIZURI

    Na Sada Salmin, DAR ES SALAAM
    KAIMU Kocha Mkuu wa Simba SC, Mrundi Masoud Juma amesema kiungo Kakule Mugheni Fabrice aliyejiunga na timu hiyo juzi atasaidia kulingana na uwezo wake 
    Akizungumza na Bin Zubeiry Sports – Online wakati wa mazoezi ya timu hiyo leo Uwanja wa Boko Veterani, ambayo Fabrice alishiriki, Masoud alisema kwamba Mkongo huyo ameonyesha uwezo wa kuridhisha na anaweza kuisaidia timu.
    Juma amesema kwamba haihitaji muda mrefu kumbaini mchezaji mzuri na ndiyo maana yeye baada ya mazoezi ya siku moja amekubali Fabrice ni mchezaji mzuri.
    Kiungo huyo aliwasili juzi usiku na kujiunga na wenzake na kuonyesha uwezo katika mazoezi hayo na Juma amesema anamfahamu kiungo huyo, ana amini atasaidia timu.
    akule Mugheni Fabrice akiwa mazoezini na Simba SC leo Uwanja wa Boko Veterani, Dar es Salaam  

    Wakati huo huo: Kuelekea maandalizi ya Nusu Fainali Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Daktari wa Simba, Yassin Gembe, amesema mshambuliaji Adam Salamba anaendelea vizuri.
    Salama alitoka nje anachechemea dakika ya 59 baada ya kuumia katika mchezo wa Robo Fainali nafasi yake ikichukuliwa na Mohammed Rashid aliyekwenda kufunga bao pekee dakika sita baadaye, Simba SC ikishinda 1-0 dhidi ya AS Ports na kwenda Nusu Fainali.
    Na kulikuwa kuna hofu mchezaji huyo aliyesajiliwa kutoka Lipuli ya Iringa mwezi uliopita atakosekana kwenye Nusu Fainali Jumatano, ambayo Simba itamenyana na JKU ya Zanzibar iliyoitoa kwa penalti 4-3 Singida United leo kufuatia sare ya 0-0 usiku wa leo Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.
    Mbali na JKU kukutana na Simba SC Jumatano – Nusu Fainali nyingine siku, mabingwa watetezi, Azam FC watamenyana na Gor Mahia Uwanja wa Taifa pia.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: KOCHA MASOUD JUMA AMSIFU KIUNGO MPYA MKONGO, ASEMA ATAISAIDIA SIMBA KUFANYA VIZURI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top