• HABARI MPYA

  Alhamisi, Aprili 19, 2018

  YANGA SC YAWEZA KUKUTANA NA WAPINZANI WAO WA 1998 LIGI YA MABINGWA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC inaweza kukutana na wapinzani wake wa mwaka 1998 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Raja Cassablanca ya Morocco baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Yanga SC imefanikiwa kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika pamoja na kufungwa 1-0 na wenyeji, Wolaita Dicha jana katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa kuwania kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika Uwanja wa Hawassa mjini Hawassa nchini Ethiopia.
  Yanga SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 7 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Yanga SC imesonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kushinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Aprili 7 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam

  Droo ya kupanga makundi manne ya michuano hiyo itafanyika Jumamosi Aprili 21 makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri kuanzia Saa 8:00 mchana.
  Na timu zilizofuzu hatua hiyo ni pamoja nan ne kutoka Kaskazini mwa Afrika; USM Alger ya Algeria, El Masry ya Misri, RS Berkane na Raja Club Athletic, maarufu Raja Casablanca za Morocco.  
  Nyingine ni AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), CARA ya Kongo, El Hilal ya Sudan, Gor Mahia ya Kenya, UD Songo ya Msumbiji, Enyimba ya Nigeria, Aduana Stars ya Ghana, Williamsville  ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali na Rayon Sports ya Rwanda.
  Yanga SC inatarajiwa kurejea nchini Saa 7:00 usiku wa leo kutoka Hawassa na kesho itaunganisha safari kwenda Mbeya kwa mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine Jumapili.
  Mwaka 1998, Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikapangwa na Rajam, Manning Rangers ya Afrika Kusini na ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Mechi ya kwanza Casablanca Yanga ilifungwa 6-1 na marudiano ilitoa sare ya 3-3 Dar es Salaam. 
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA SC YAWEZA KUKUTANA NA WAPINZANI WAO WA 1998 LIGI YA MABINGWA RAJA CASABLANCA YA MOROCCO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top