• HABARI MPYA

  Ijumaa, Aprili 20, 2018

  YANGA YAREJEA DAR, KESHO KUUNGANISHA SAFARI KWA NDEGE TENA KUIFUATA MBEYA CITY

  Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
  YANGA SC imerejea jana kutoka Ethiopia ambako imefuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuwatoa wenyeji, Wolaita Dicha kwa jumla ya mabao 2-1 ikishinda 2-0 nyumbani Aprili 7, kabla ya kufungwa 1-0 juzi mjini Hawassa.
  Yanga iliwasili Saa 7:40 na usiku wa jana na kupokewa na mamia na ya mashabiki wake waliojitokeza kuipongeza timu yao kwa kwa kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu.
  Na Kikosi cha Yanga SC kimekwenda moja kwa moja kambini tayari kwa safari ya ndege tena kwenda Mbeya kesho kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara dhidi ya wenyeji, Mbeya City Uwanja wa Sokoine.
  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh anatarajiwa kuondoka Dar es Salaam usiku wa leo, kwenda Cairo nchini Misri kuiwakilisha klabu katika droo ya makundi na ratiba ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika. 
  Yanga SC inaweza kukutana na wapinzani wake wa mwaka 1998 kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Raja Cassablanca ya Morocco baada ya kufuzu hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika.
  Droo ya kupanga makundi manne ya michuano hiyo itafanyika Jumamosi Aprili 21 makao makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) mjini Cairo, Misri kuanzia Saa 8:00 mchana.
  Na timu zilizofuzu hatua hiyo ni pamoja nan ne kutoka Kaskazini mwa Afrika; USM Alger ya Algeria, El Masry ya Misri, RS Berkane na Raja Club Athletic, maarufu Raja Casablanca za Morocco.  
  Nyingine ni AS Vita ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), CARA ya Kongo, El Hilal ya Sudan, Gor Mahia ya Kenya, UD Songo ya Msumbiji, Enyimba ya Nigeria, Aduana Stars ya Ghana, Williamsville  ya Ivory Coast, Djoliba ya Mali na Rayon Sports ya Rwanda.
  Mwaka 1998, Yanga ilifuzu hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika na ikapangwa na Raja, Manning Rangers ya Afrika Kusini na ASEC Mimosas ya Ivory Coast. Mechi ya kwanza Casablanca Yanga ilifungwa 6-1 na marudiano ilitoa sare ya 3-3 Dar es Salaam.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: YANGA YAREJEA DAR, KESHO KUUNGANISHA SAFARI KWA NDEGE TENA KUIFUATA MBEYA CITY Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top