• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 22, 2018

  KING KIBADENI MWENYE REKODI YA KIPEKEE MECHI ZA MAHASIMU WA JADI, SIMBA NA YANGA

  Mshambuliaji wa Simba SC, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibaden’ akiwa na mpira wake enzi zake miaka ya 1970, kipindi ambacho aliweka rekodi ya kufunga mabao matatu katika mechi moja dhidi ya mahasimu wa jadi, Yanga SC kwenye ushindi wa 6-0  Julai 19, mwaka 1977 Uwanja wa Taifa, sasa Uhuru mjini Dar es Salaam. Kibadeni alifunga dakika za 10, 42 na 89 wakati mabao mengine yalifungwa na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na beki wa Yanga, Suleiman Sanga aliyejifunga dakika ya 20.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: KING KIBADENI MWENYE REKODI YA KIPEKEE MECHI ZA MAHASIMU WA JADI, SIMBA NA YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top