• HABARI MPYA

  Jumapili, Aprili 29, 2018

  VIKOSI VINAVYOANZA HADI WA BENCHI SIMBA NA YANGA LEO

  Papy Kabamba Tshishimbi (kulia) na Shiza Kichuya (kushoto) wanakutana tena uwanjani leo
  TIMU zote mbili, Simba SC na Yanga SC zimeweka hadharani vikosi vyake kuelekea mpambano wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara unaotarajiwa kuanza Saa 10:00 jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
  Mchezo huo utachezeshwa na refa Emmanuel Mwandembwa wa Arusha atakayesaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Mohammed Mkono wa Tanga, wakati refa wa akiba atakuwa Heri Sasii pia wa Dar es Salaam. 
  Simba SC; Aishi Manula, Nicholas Gyan, Asante Kwasi, Erasto Nyoni, Yussuf Mlipili, James Kotei, Jonas Mkude, Shomary Kapombe, John Bocco, Emmanuel Okwi na Shiza Kichuya.
  Benchi; Said Mohammed 'Nduda', Paul Bukaba, Said Ndemla, Mohammed Hussein 'Tshabalala', Muzamil Yassin, Laudit Mavugo na Rashid Juma.
  Yanga SC; Youthe Rostand, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Andrew Vincent 'Dante', Kelvin Yondan, Said Juma 'Makapu', Yussuf Mhilu, Papy Kabamba Tshishimbi, Obrey Chirwa, Raphael Daudi na Ibrahim Ajib.
  Benchi; Ramadhani Kabwili, Juma Abdul, Abdallah Shaibu 'Ninja', Maka Edward, Juma Mahadhi, Pius Buswita na Emmanuel Martin.
  • Blogger Comments
  • Facebook Comments

  0 maoni:

  Item Reviewed: VIKOSI VINAVYOANZA HADI WA BENCHI SIMBA NA YANGA LEO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
  Scroll to Top